loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge wa Busega kukabili wanaopora fedha za miradi

Dk Kamani aliyasema hayo juzi wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara, katika kijiji cha Mwabulanja, Nassa Jeneri, wilayani Busega.

“Nitakuwa mkali kwa watu wote wanaokula fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi, sitamvumilia mtu yeyote katika hilo,” alisema.

Alimwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, madiwani na watendaji wote kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa jimboni humo.

Alisema katika kuunga mkono nguvu za wananchi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya elimu, maji na miundombinu.

Katika ziara yake hiyo, Dk Kamani aliahidi kutoa mabati 100 kwa ajili ya kuezekea vyumba viwili vya madarasa katika shule moja ya msingi na mabati kujengea ofisi moja ya kijiji jimboni humo .

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Ahmed Makongo, Simiyu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi