loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mbunge wa Kibakwe ataka wananchi kumuunga mkono Rais

Alitoa kauli hiyo juzi katika Kijiji cha Gulwe Wilaya ya Mpwapwa ambapo pia rais Kikwete alizungumza na wananchi Mbunge huyo alisema kwa kipindi ambacho Rais Jakaya Kikwete amekuwa madarakani kumekuwa na msukumo mkubwa wa maendeleo katika nyanja za miundombinu, elimu, afya.

Alisema tangu nchi ipate uhuru hadi 2005 jimbo hilo lilikuwa na zahanati 16 lakini sasa zimeongezeka zahanati mpya 21 na kufanya idadi ya zahanati kuwa 37 na sasa wamebakiza zahanati 12 ili kufikia malengo.

Pia alisema hata shule za sekondari zimeongezeka kutoka tatu na kufikia sekondari 13 huku zikiwa na walimu wasiopungua 10 kila shule.

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto kubwa ya nyumba za walimu na maabara hasa kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi.

Alisema jimbo hilo kutokana na kujiimarisha katika nyanja ya elimu imeweza kupeleka watoto wengi vyuo vikuu ambapo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kuna wanafunzi 147 wanaotoka katika Jimbo la Kibakwe na wengi wamesoma katika shule za kata.

Alisema hata katika mawasiliano mwaka 2005 kulikuwa hakuna mnara hata moja wa simu lakini sasa mawasiliano yamefikia asilimia 75 na kuna minara tisa ya simu.

Pia alisema katika maeneo ya Ipele, Mzondozi, Wota na Rudi kuna ujenzi wa miradi minne ya minara ya simu.

Akizungumzia miundombinu alisema kazi kubwa imefanyika kufungua barabara na sasa anatumaini lengo la Serikali kujenga barabara kutoka Mbande hadi Kibakwe litafungua milango mipana ya maendeleo.

Alisema wakala wa barabara mkoani Dodoma Mhandisi Leonard Chimagu amekuwa akifanya kazi nzuri na daraja la Gulwe litaiunganisha Mpwapwa na Kibakwe na kumaliza tatizo la mawasiliano maeneo hayo hasa wakati wa mvua.

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi