loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge : Wanawake msibweteke

Badala yake, amewataka wajiunge na vikundi vya kuweka na kukopa (VICOBA), ili kuwawezesha kuendesha biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Magige aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, alipozungumza na wanawake wajasiriamali wadogo kutoka Soko la Kilombero katika semina ya kuwajengea uwezo na jinsi ya kujiunga na VICOBA, ili waweze kujitegemea katika familia zao.

Aidha, katika semina hiyo, mbunge huyo, alikabidhi Sh milioni 1.5 na vifaa mbalimbali vya upishi kwa vikundi vitano vya wanawake wajasiriamali vilivyopo mkoani hapa.

Akizungumza katika semina hiyo, alisema amekuwa akiwasaidia wanawake wajasiriamali mkoani humo, kwa kuwapatia vitendea kazi na fedha, lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kutokuwa tegemezi katika familia zao.

Pia, Magige aliwasaidia wanawake hao wajasiriamali takribani 105 kupata elimu juu ya namna ya kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa, vitakavyowainua kiuchumi na kuwakwamua na umasikini.

“Wanawake wengi wana moyo wa kujituma katika shughuli za kiuchumi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa elimu na jinsi ya kujiendeleza kibiashara,” alisema Magige.

Alisema tangu ameanzisha utaratibu wa kuwasaidia wanawake wajasiriamali, wanaojishughulisha na biashara ndogo, wengi wao wameweza kujikwamua kiuchumi kwa kupata kipato, ikiwemo kusomesha watoto wao, kula lishe bora na kulipa kodi za nyumba, hivyo kupunguza tatizo la unyanyapaa katika familia zao.

Akizungumzia elimu hiyo aliyoipata, mmoja wa wanawake hao wajasiriamali, Rehema Maneno alisema kuwa hapo awali alikuwa hana uelewa wowote wa kujiunga na vikundi ila kupitia elimu aliyoipata naye amehamasika kujiunga na Vicoba.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi