loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Membe apongeza Kanisa Katoliki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuchanguliwa kwa Papa Francis iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Francisco Montecillo Padilla.

Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini, mapadri, watawa, mabalozi waliopo Tanzania na wageni waalikwa.

Membe alisema Serikali imedhamiria kudumisha usalama wa Watanzania wote pamoja na amani na utulivu nchini kote kwa gharama yoyote.

“Kamwe hakutakuwa na amani kama hakuna uhuru wa kuabudu ambao imelezwa kwenye katiba,” alisema.

Aliongeza: “ Serikali inaamini kuwa kanisa kamilifu jukumu lake ni kutia moyo Watanzania katika kusamehe na kuwapenda wengine licha ya tofauti za kidini.”

Membe aliwakumbusha wageni waalikwa kuwa Papa Francis alihubiri kuhusu amani, upendo na jukumu la kulinda haki za walio wachache wakati wa mahubiri aliyoyatoa Vatican Mei 19, mwaka jana. Awali, Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Francisco Montecillo Padilla amesifia kiongozi wa Kanisa Katoliki kuwa ni ‘ Papa wa Masikini”

“Siku zote Papa Francis amekuwa akitoa wito kwa viongozi wa dini wa madhehebu yote wa kulinda zawadi na utajili wa Mungu, watoto na binadamu wote.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi