loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Meya Silaa kutia baraka Klabu Bingwa Kikapu

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Salehe Zonga alisema kuelekea mashindano hayo tayari timu 31 zimethibitisha ushiriki wao.

Baadhi ya timu hizo ni Morogoro, Bandari, King United kutoka Tanga, Jeshi Stars, JKT, Kurasini Hits, Musoma, Lindi, Mtwara, Jogoo, Pazi, Oilers, Ilala Flats, Wailes, PTW, Mzinga, Mipango Dodoma, ABC wanaume, UDOM, Risasi na Shinyanga.

Zonga alisema idadi ya timu shiriki itaongezeka kwani timu bado zinaendelea kuthibitisha ushiriki wao.

“Maandalizi yanakwenda vizuri, tumejipanga wenyewe na hata kama hatutakuwa na wafadhili tutahakikisha kwamba tunafanikisha kama ambavyo tumepanga,”alisema.

Alisema hamasa ya timu kujitokeza imekuwa kubwa ukilinganisha na miaka minne iliyopita, kwani baadhi ya timu za mikoani hazikuonesha nia kwa muda mrefu kutokana na matatizo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mchezo huo.

Zonga alisema wachezaji watakaofanya vizuri kwenye michuano hiyo watachukuliwa kwa ajili ya akiba kwenye timu ya Taifa na mashindano mengine ya umri kuanzia chini ya miaka 18 yatakayoanzishwa siku za karibuni.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi