loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfumo himaya moja ya forodha kuanza karibuni

Utekelezaji wa mfumo huu unafanyika kutokana na kubainika kuwa na mafanikio makubwa baada ya majaribio yake kufanyika tangu Julai mwaka jana.

Unalenga kupunguza gharama na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, hali ambayo itavutia uwekezaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.

Inakadiriwa kuwa mfumo huo utakapotekelezwa kwa asilimia 100 , zaidi ya asilimia 70 ya gharama za kufanya biashara zitakuwa zimeondolewa.

Naibu Kamishna Mkuu wa Forodha (Uwezeshaji Biashara), Patrick Mugoya alisema hayo jana wakati wa mahojiano maalumu juu ya utekelezaji wa mfumo wa himaya moja ya forodha.

Alisema katika kipindi hiki cha majaribio, pamejitokeza changamoto kadhaa katika utekelezaji wa mfumo huu lakini hatua zimechukuliwa kutafuta suluhisho la matatizo haya kabla ya mwezi wa nne mwaka huu kwa ajili ya kutumika rasmi kwa mfumo huu mwaka wa fedha ujao.

“Tumefikia hatua nzuri katika kutatua changamoto hizi ili kufanya utekelezaji wa mfumo huu uwe na manufaa tarajiwa na kuwezesha biashara ifanyike katika mazingira stahiki na ya gharama nafuu,” alisema.

Baadhi ya changamoto ambazo zinafanyiwa kazi na wataalamu wa forodha kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na kutokuwa na mwingiliano wa mifumo ya forodha katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hofu kwa maofisa wa forodha kupoteza kazi kutokana na mfumo mpya.

Nyingine ni pamoja na taasisi za udhibiti katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni wadau wa karibu katika kufanikisha shughuli za forodha kutoupokea haraka mfumo huu wa himaya moja.

Alisema katika utekelezaji wa mfumo huu, mchakato wa kuandaa nyaraka za kutoa mizigo bandarini hufanyika katika nchi ambayo mzigo huo hupelekwa na hasa baada ya kupokea kibali maalumu kutoka kwenye bandari ambapo mzigo umefikia.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi