loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfumo wa kusajili mifugo wazinduliwa

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani alizindua mfumo huo jana eneo la Mlandizi wilayani Kibaha na kuongeza kuwa mfumo huo ni nyenzo muhimu na ya lazima katika ufugaji kwa sasa duniani kote ili kuwezesha kukubalika katika masoko ya kimataifa.

Aliwaelekeza wafugaji wote katika maeneo ambayo yatatangazwa kuwa ya utambuzi wa mifugo kushiriki katika kutambua na kusajii mifugo yao na kuwa tayari kuchangia katika ununuzi wa vifaa vya utambuzi wa mifugo hiyo.

Alisema uzinduzi wa mfumo huo ni nyenzo inayosaidia kukabiliana na magonjwa ya mifugo, wizi wa mifugo, uhamishaji au usafirishaji holela wa mifugo na kuepusha migogoro baina ya wafugaji na wakulima pamoja na watumiaji wengine wa ardhi.

Alisema utaratibu wa kuweka kumbukumbu ndiyo usajili wa mifugo, wafugaji na matukio muhimu ya mifugo kama kuzaliwa, vifo, kupotea, kuhama au kusafirisha, chanjo au matibabu mengine ilikuwezesha kufuatiliwa.

Dk Kamani alisema katika kuhakikisha mfumo huo unazinduliwa, Tanzania ilipata msaada wa dola za Marekani 475,000 (sawa na Sh milioni 781.37) kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ambao walisaidia kujenga mfumo huo.

Alisema mfumo huo kwa sasa umekamilika na umeanza kufanya kazi katika wilaya za mfano kama Kibaha, Bagamoyo na Muheza, ambapo jumla ya ng’ombe 5,845 zimetambuliwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania Kanda ya Pwani, Mohamed Hamis alisisitiza kutolewa kwa elimu ya kutosha kwa wafugaji ili waweze kufahamu athari na mafanikio ya mfumo huo kabla ya kuanza kutekeleza.

 

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi