loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfumuko wa bei wafikia asilimia 6.7

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hayo juzi na kuongeza kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Agosti mwaka huu, imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Julai.

Aidha alisema fahirisi za bei imeongezeka hadi 149.31 Agosti kutoka 149.16 Julai mwaka huu ambapo pia alitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi, kuwa ni bia kwa asilimia 2.5, sare za shule kwa asilimia 1.5, mkaa kwa asilimia 1.1 na samani kwa asilimia 2.4.

Nyingine ni bidhaa za jamii ya kitambaa kwa matumizi ya nyumbani kwa asilimia 1.5, huduma za meno asilimia 1.0, huduma ya chakula kwenye migahawa asilimia 0.4 na huduma ya kulala hotelini asilimia 1.4.

“Kwa ujumla mfumuko wa bei una mwelekeo unaofanana na nchi nyingine za Afrika Mashariki mfano mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka hadi asilimia 8.36 Agosti mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7.67 Julai mwaka huu,” alisema.

Alisema kwa upande mwingine mfumuko wa bei nchini Uganda umeendelea kupungua hadi asilimia 2.8 Agosti 2014 kutoka asilimia 4.3 Julai, mwaka huu.

Alitoa mwito wa wanahabari kuwaelimisha watunga sera na wananchi wote kwa ujumla kuhusu umuhimu wa matumizi ya takwimu hizo za bei pamoja na nyinginezo zinazotolewa na NBS.

Pia aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ofisi za Takwimu za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi