loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mholanzi wa Yanga tambo kibao

Akizungumza na gazeti hili, kocha huyo mpya aliyerithi mikoba ya Mholanzi mwenzake aliyetimuliwa, Ernie Brandts, alisema anakiona kikosi chake kipo katika hali nzuri kimchezo wa leo na ligi nzima kiujumla.

Van der Pluijm alisema kutokana na mazoezi waliyofanya nchini Uturuki ambako walipiga kambi kwa wiki mbili, yamewapa imani ya kufanya vema katika michezo yote ya ligi.

Alisema akishirikiana na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa, wachezaji wa kikosi hicho wamenolewa katika kila idara kuanzia ushambuliaji, ulinzi na wamefuzu kushiriki vema ligi hiyo.

“Wachezaji wapo katika hali nzuri na hakuna majeraha na tunataka kuona kuwa kila kitu kinaenda sawa na kutetea ubingwa wetu katika mzunguko huu wa pili,” alisema Van der Pluijm, kocha wa zamani wa timu ya Berekem Chelsea ya Ghana.

Katika hatua nyingine, Yanga imeeleza kukatishwa tamaa na hatua ya kuzuiliwa kwa mchezaji Emmanuel Okwi wakati dirisha la usajili likiwa limefungwa.

Taarifa hiyo imeweka wazi hati ya uhamisho na mawasiliano yaliyofanyika kati ya klabu hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Taarifa hiyo ilielezea kuwa uongozi wa Yanga umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda ambaye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imemzuia kuichezea Yanga mpaka watakapopata ufafanuzi kutoka FIFA.

Ilifafanua kuwa Yanga ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Desemba 15, 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) iliyowasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu.

Ilionesha kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo, TFF ilipitisha jina lake kwa kuwapa leseni namba 921225001 iliyomruhusu mchezaji kuichezea Yanga na kisha kuituma CAF Desemba 31, 2013 kwa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Yanga kwa mashindano hayo.

Akifafanua, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kiziguto alihoji uhalali wa Kamati ya TFF kuchukua uamuzi huo sasa wakati ilikuwa na muda wa kutosha tangu Desemba 15, mwaka jana ambapo usajili ulikamilika.

“Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans, ilhali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans,” alihoji Kizuguto.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Evance Ng'ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi