Mtu huyu alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa kwa shtaka la kupanda miche ya bangi shambani kwake. Hakimu wa Mahakama hiyo, Ramadhan Rugemalira alimwamchia huru mshitakiwa huyo baada ya kulipa faini .
Kwa mujibu wa hati za mashtaka, mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 6,mwaka huu mchana kijijini Mtapenda.
Awali mshitakiwa huyo alikana mashitaka lakini juzi wakati akisomewa maelezo ya awali mahakamani hapo baada ya mashahidi upande wa mashtaka ukiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi , Hasmimu Gwelo kutoa ushahidi wao, mshtakiwa alikiri kosa lake mahakamani hapa.
Akijitetea mahakamani hapo mshatakiwa huyo alikiri kuwa alikuwa hajui kama ni haramu kulima bangi isitoshe ilikuwa ikimpatia kipato cha kutosha kumwezesha kuwalea wazazi wake ambao ni wazee na watoto wake watatu.