loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mikikimikiki ya kisiasa mwaka 2013

Mikikimikiki ya kisiasa mwaka 2013

Lakini pia unafungwa kwa Rais kurekebisha Baraza la Mawaziri kutokana na kutengua uteuzi wa mawaziri wanne walioshindwa kusimamia wizara zao katika Operesheni ya Tokomeza Ujangili nchini. Jambo hilo kubwa kisiasa, safari hii likianzia bungeni, kupitia ripoti ya Mbunge wa Kahama, Lembeli, baadhi mawaziri waliongoza kampeni ya tokomeza ujangili, wametenguliwa uwaziri wao.

Mwaka unafungwa kwa mawaziri wanne kutenguliwa uteuzi wao ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David.

Kutengua uteuzi wa mawaziri wanne, kumetokana na kauli yake wakati anafungua mwaka 2013, kwamba ….’Tutaendelea kuimarisha utendaji kazi serikalini na kuhimiza uwajibikaji katika ngazi zote za uongozi.

” Pamoja na mawaziri hao, Serikali imeendelea kuwaondoa baadhi ya watendaji wabovu katika ngazi zingine serikalini, kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda alivyotoa taarifa bungeni wakati akiahirisha Bunge hilo mwaka huu. Tukio moja la kufungia mwaka, Rais Kikwete ametengua rasmi uteuzi wa mawaziri wanne waliotuhumiwa kutosimamia wizara zao kutokana na makosa ya ukiukwaji wa haki za kiraia wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili iliyokuwa ikiendeshwa na Serikali.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesoma bungeni mjini Dodoma, taarifa ya Rais kwamba ameridhia maoni ya wabunge wakati wa kujadili ripoti ya Kamati iliyoundwa na kuongozwa na Mbunge James Lembeli kuwa mawaziri wanne waliotuhumiwa waondoke. Hata hivyo, Rais Jakaya Kikwete atakumbukwa mwaka huu ni kwamba amesimamia hoja ya mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoundwa tarehe 1 Mei, 2012 ilianza kazi yake rasmi tarehe 29 Juni, 2012 na inaendelea vyema. Rais amesimamia kwa nguvu zake kwa kushirikisha vyama vya siasa na makundi mbalimbali katika kuandaa rasmi. Katika mchakato huo, Tume ya Marekebisho ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, imetoa mchango mkubwa, na wakati ikiendelea na kazi mjumbe wake, Dk Sengondo Mvungi amepoteza maisha.

Tangu Januari mwaka huu, ilikuwa ikikusanya maoni ya makundi maalumu na baada ya hatua kukamilika Tume imeandaa Rasimu ya Katiba. Hivi sasa Rais ametoa idhini ya makundi, kuwasilisha majina ya kuunda Bunge la Katiba. Japokuwa katika suala hilo, Vyama vya upinzani Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, kwa mara ya kwanza vimeungana kumtaka Rais Kikwete asisaini muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba wa 2013 kwa madai kwamba imepitishwa bila kujadiliwa.

Viongozi hao wamekutana na Rais Ikulu kujadili jambo hilo, wakafikia muafaka. Rasimu hiyo kwa mara nyingine, iliwafikisha viongozi hao hadi Ikulu kuzungumza na Rais Kikwete ili kupata muafaka, ambao haukumzuia kusaini, isipokuwa alitoa fursa kuongeza vipengele ambavyo wanadhani havijaingia kwenye rasimu.

Katika kuhakikisha maandalizi ya Katiba mpya yanaendelea, Rais amesimamia na hivi sasa makundi mbalimbali yamepewa fursa ya kuteua wajumbe wa kuingia kwenye Bunge la Katiba. Ujio wa wageni Pia Tanzania imeendelea kuwa karimu kwa wageni, Rais pamoja na Watanzania wote kwa ujumla wamekuwa wenyeji wa viongozi mbalimbali duniani.

Rais wa China, Xi Jing Ping alipokewa mapema mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine, alisaini mikataba kadhaa na Serikali. Baadaye Tanzania ilikuwa na ugeni mzito wa Rais wa Marekani, Baraka Obama Julai mosi mwaka huu. Katika nchi nne alizotembelea Afrika, ikiwamo Senegal, Afrika Kusini na Ghana pamoja na Tanzania.

Wakati huo akiwa nchini marais wengine wa Marekani walikuwapo, George Bush na Bill Clinton. Mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali unaojulikana kama Global 2013 Smart Partnership Dialogue ulifanyika Dar es Salaam. Mkutano huu ulikutanisha viongozi wa Serikali wakiwemo wakuu wa nchi na Serikali, viongozi wa sekta binafsi wakiwemo wa kampuni kubwa za kimataifa, wasomi na wawakilishi wa asasi za kiraia na watu binafsi akiwamo, Mfalme Mswati wa III.

Mkutano huo ulioshirikisha watu 500 umezungumzia “Matumizi ya Sayansi na Teknolojia kwa Ajili ya Maendeleo ya Afrika.” Pamoja na kuwa mwenyeji lakini pia imedumisha ushirikiano na kusimamia kutatua migogoro mbalimbali. Moja ya mgogoro mkubwa ulikuwa baina ya Tanzania na Malawi ulioibuka kuhusu mpaka wa nchi mbili hizo katika Ziwa Nyasa.

Rais kwa kushirikiana na Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe amekuwa mstari wa mbele katika kutatua mgogoro huo. Rais amejitahidi kutafuta suluhu ya mgogoro wa Rwanda ambayo ni nchi moja miongoni mwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao ulikuwa unaelekea kuzitenga nchi za Burundi na Tanzania na upande wa pili kuziacha, Rwanda, Kenya na Uganda.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakati Rais Kikwete akijitahidi katika kuleta amani ndani na nje ya Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni Mwenyekiti wake, kimetumia maazimio ya Mkutano Mkuu wa chama hicho, uliofanyika Novemba mwaka juzi, kwamba na kutekeleza maazimio ya chama kuisimamia Serikali.

Kutokana na maazimio hayo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Asha- Rose Migiro wamesimama kidete na wamekuwa mstari wa mbele katika ziara zao mikoani na kuonesha viongozi wabovu wakiwamo mawaziri.

Katika hatua hiyo, baadhi ya mawaziri wamewatuhumu kwamba hawajawajibika vya kutosha na hivyo wakaitwa mbele ya Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Saada Mkuya kwa niaba ya Waziri wa Fedha. Dk William Mgimwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, Waziri wa Utumishi, Celina Kombani, Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopha Chizza.

Viongozi hao waliwataka mawaziri hao, na wengine wafike mbele ya Kamati Kuu ya CCM, kujieleza au kutoa maelezo kuhusu utendaji wao na kwanini hawawajibiki kutatua kero za wakulima wa mazao mbalimbali ikiwamo pamba, tumbaku, kahawa na wananchi katika maeneo mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa malalamiko ya wazi kuhusu utendaji wao hafifu.

Chama Cha Wananchi (CUF) CUF imeingia kwenye matukio mwaka huu. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amemtangaza Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu, 2015.

Kutangaza jambo hilo, mapema mwaka huu, kunamfanya Profesa Lipumba aendelee kuwa mgombea wa urais kwa mara nyingine na kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa muda mrefu zaidi ya miaka 10. CUF pia imewatangazia neema Watanzania kwamba endapo itachukua madaraka katika Uchaguzi Mkuu huo itawajaza fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaondolea umasikini.

Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, Hamad amesema hayo katika Mkutano wa Uzinduzi wa Oparesheni ya Mchakamchaka (V4) kuelekea mwaka 2015, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro. Kitendo hicho, kilimfanya Hamad naye atangaze kwamba anaweza kuendelea kugombea maadamu afya itaendelea kumruhusu.

Hivyo hadi sasa kinachoonekana kisiasa ni kwamba viongozi hao wawili, wataendelea kugombea nafasi zao hadi pale ambapo afya zao zitakuwa mbaya au haziwaruhusu waendelee. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Sambamba na CUF, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa atapewa fursa ya kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Mbowe amesema: “Kama Mwenyezi Mungu atampa uhai na kuwa na afya njema hadi mwaka 2015, Dk Slaa anatosha Chadema, tutampa fursa nyingine ya kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya urais.” Wakati hayo yakiendelea, Chadema iliingia katika mtafaruku mkubwa wa kuwavua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na kiongozi wa Kamati Kuu, Dk Mkumbo Kitila.

Katika kampeni hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilibroad Slaa, wakisema uamuzi huo unatokan a na maamuzi ya Kamati Kuu (CC). K a - mati hiyo imesema kwamba Z i t t o na Kitila wanatuhum i w a kufanya harakati za kutaka kukihujumu chama hicho pamoja na kwenda kinyume na uamuzi wa chama na mwenendo wake.

Zitto amepoteza nafasi yake ya Unaibu Katibu Mkuu na Unaibu Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, huku Mkumbo Kitila amevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu katika chama.

Zitto ambaye ni kiongozi kijana amefanya mengi katika mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kupigania kurudishwa mabilioni ya fedha yaliofichwa Uswisi jambo lililomuongezea maadui ndani na nje ya chama chake japokuwa bado fedha hizo hazijarudishwa na wala hawajulikani walioficha fedha hizo.

Amesimamia hoja ya kukaguliwa matumizi ya ruzuku ndani ya vyama vya siasa kikiwemo Chadema. Mara mbili amewahi, kusimamia hoja ya kumng’oa Waziri Mkuu kutokana na utendaji mbovu na hatimaye wakawajibishwa mawaziri kadhaa walioonekana wana matatizo katika utendaji wao.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kama kiongozi mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni naye amekuwa kichocheo katika shughuli mbalimbali ndani ya chama pamoja na Katibu Mkuu, Dk Wilibroad Slaa.

Lakini viongozi wengine wa upinzani waliovuma mwaka huu ni pamoja na James Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba nao wamekuwa kivutio kikubwa katika mwaka huu, hasa kitendo cha viongozi wa vyama vya upinzani Chadema, CUF na NCCRMageuzi kwa umoja wao kumtaka Rais Kikwete asisaini muswada wa marekebisho ya Katiba.

Upande wa Serikali na chama chake, kutenguliwa uteuzi wa mawaziri wanne, kunampa nafasi Rais Kikwete kufanya marekebisho Baraza lake la Mawaziri. Hilo ndio tukio la mwaka, limezua gumzo nani atakuwapo na nani ataondolewa wakiwamo hao waliotengul i w a . T u k i o hilo ni c h i m - b u k o la mageuzi mengi yatakayofuata kuhusu watendaji wabovu.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi