loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Miradi ya UN nchini yasaidiwa bil. 42/-

Makubaliano ya fedha hizo yametiwa saini kati ya Balozi wa Sweden, Lennarth Hjelmaker na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez.

Fedha hizo sawa na dola milioni 24 zinaelekezwa katika miradi ya UNDAP inayokubaliana na sera za Sweden za kuwezesha utawala bora, ustawi wa jamii na wanawake na watoto na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden fedha zitasaidia utekelezaji wa mipango ya Mkukuta, Mkuza na Matokeo makubwa sasa (BRN) inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Alisema ni matumaini yake kuwa fedha hizo zitaboresha hali ya kufanya biashara, kuwekeza kwa lengo la kutoa ajira zaidi, kuwezesha uchaguzi huru, kuimarisha huduma za jamii, kuimarisha mipango, uwajibikaji na kuimarisha mawasiliano ya radio kwa ajili ya upashanaji habari vijijini ili kusaidia maamuzi yenye mtazamo mpana zaidi miongoni mwa watu wa vijijini.

Katika hafla hiyo Balozi wa Sweden alisema pamoja na kutoa fedha hizo kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa bado, nchi yake itaendelea na makubaliano yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania na kuendelea kutoa misaada yake ya kimaendeleo.

Balozi huyo alisema hayo akijibu swali la kwanini wanatoa fedha kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa pekee na kama wameacha kutoa misaada ya moja kwa moja serikalini.

Aidha Balozi Lennarth Hjelmåker alisema kwamba Tanzania imekuwa mfano bora kabisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwezesha ufanisi mkubwa wa miradi ya maendeleo yaliyolenga kuwawezesha Watanzania kupiga hatua mbele na kuhakikisha kuwapo kwa amani.

Alisema misaada ya taifa hilo imelenga kupata matokeo yanayotakiwa na kwamba itaendelea kusaidia pia taasisi nyingine zisizo za kiserikali na serikali yenyewe. Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez, ameishukuru Sweden kwa kuendelea kuwa mshirika wa maendeleo.

RAIS John Magufuli ameagiza utoroshaji wa magogo kwenda nje na ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi