loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mitambo ya mafuta kuzimwa

Kutokana na hatua hiyo, serikali itaokoa zaidi ya bilioni 300 kutokana na uzalishaji huo kutumia Sh trilioni 1.6 kuzalisha umeme wa megawati 350.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha ziara ya kukagua bomba la gesi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue na makatibu wakuu wengine 12 wa wizara mbalimbali walitembelea mtambo wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, jijini.

Alisema mwishoni mwa mwaka ndipo mitambo hiyo itasitishwa na wakati huo, mtambo wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi One, bomba la kusafirisha gesi asilia nalo litakuwa limekamilika.

Pia mtambo wa megawati 200 ulioko Ubungo ambao hauzalishi umeme kutokana na uhaba wa gesi, ifikapo mwishoni mwa mwaka utakuwa umeanza kazi.

Maswi alisema baada ya kusitishwa kwa matumizi ya kampuni hizo za mafuta, majenereta hayo yanaweza kubaki kwa dharura.

Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo ya siku mbili iliyoanzia mkoani Mtwara, Sefue alisema ameridhishwa kwa kasi ya ujenzi wa bomba hilo la gesi kwani limeendana na madhumuni ya Matokeo Makubwa Sasa.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi