loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mizinga Melu aula Barclays Africa Group

Akizungumzia uteuzi huo, Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa Group, Maria Ramos, alieleza kufurahishwa na uteuzi huo.

“Nimefurahi sana kwamba tumeweza kumteua mtu mwenye uelewa mkubwa na utaalamu katika shughuli hii. Uteuzi wake utasaidia sana kutekeleza malengo yetu barani humu,” alisema.

Melu alijiunga na Absa Group Machi mwaka jana akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NBC Tanzania, ambako anatajwa kwamba alitengeneza timu imara inayofanya mabadiliko makubwa katika biashara ya fedha.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, imesema anaondoka akiwa ameiacha NBC ikiwa imara na timu aliyoiandaa ina sehemu ya kuanzia.

Awali, aliwahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Zambia. Pia alifanya kazi katika Global Head of Development Organisations, Uingereza na Mkuu wa Taasisi za Fedha Afrika katika nchi za Afrika Kusini na Kenya.

Akiwa na Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Fedha (MBA) kutoka Henley Management School , anatajwa kuwa na uzoefu mkubwa wa kazi katika nchi nyingi za Afrika.

Wakurugenzi wakuu wote wa Barclays Africa waliopo nje ya Afrika Kusini, watawajibika kwa Mizinga, atakayeratibu mipango yote ya pamoja na kuhakikisha maendeleo ya huduma na mbinu za nchi moja moja, ikiwa ni pamoja na kuzisaidia kufanya kazi vizuri.

Mizinga atawajibika kwa David Hodnett, ambaye ni Naibu Mtendaji Mkuu wa wa Barclays Africa Group.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi