loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mke wa Rais apongeza walioacha kutumia ‘unga’

Mama Shein alisema hayo Fuoni leo wakati alipotoa msaada wa vifaa mbalimbali, ikiwemo vyakula vyenye thamani ya Sh milioni tatu kwa ajili ya mahitaji ya wanawake wanaoishi katika nyumba za kurekebisha tabia, kwa watu walioacha matumizi ya dawa za kulevya, maarufu 'sober house'.

Alisema uamuzi huo ni wa kupongezwa kwa sababu si kawaida kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha moja kwa moja.

“Nawapongezeni kwa kuchukua uamuzi wa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya...ni ujasiri mkubwa ambao unatakiwa kuungwa mkono kwa nguvu zote,” alisema.

Alisema wanawake wengi waliojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya wamepata matatizo makubwa na athari za kisaikolojia pamoja na kutengwa na familia zao.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Asha Bakari Makame, alisema dawa za kulevya ni changamoto kubwa inayolikabili Taifa la Tanzania.

“Dawa za kulevya ni janga la Taifa ambalo wanawake mnatakiwa kuepukana nalo kwa sababu athari zake ni kubwa zaidi wakati wanawake wanapokuwa na ujauzito,” alisema.

Wanawake 20 wanaishi katika nyumba ya kurekebisha tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya Sober House.

Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kutenga fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kuzisaidia nyumba hizo ambazo zimeleta mabadiliko makubwa na vijana wengi wanaoishi katika nyumba hizo kuachana na madawa hayo.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imebainisha kuwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi