loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

'Mkikaa vijiweni mtaendelea kulalamika'

Alisema hayo hivi karibuni katika mahafali ya nane ya Chuo cha Sayansi ya Afya, kilichopo Bulongwa wilayani Makete mkoani Njombe.

Chuo hicho kinamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Mchechu alisema wanatafuta njia ya mkato kufikia ndoto zao za mafanikio, wataishia kulalamika kwa kukosa kile wanachotaka, tofauti na wale wanaohangaika kujiendeleza kimaisha kwa njia halali na kwa nidhamu.

Alisema taasisi mbalimbali zinaweza kujitokeza na kusaidia katika uwekezaji kama wana Makete watashirikiana na Serikali kutangaza fursa walizonazo na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Awali, Askofu Msaidizi wa KKKT Dayosisi ya Kusini na Kati, Filimoni Kauka aliwakumbusha wahitimu hao kuzingatia maadili ya kazi yao na kuepuka vishawishi katika utoaji wa huduma.

“Kama viapo mnavyoapa wakati mnapomaliza masomo yenu na mnapoanza kazi vinavyoelekeza, tumieni viapo hivyo kama muongozo wenu wa kutoa na kuboresha huduma ya afya katika jamii,” alisema.

Askofu Kauka alisema utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa, ni jambo nyeti linalopaswa kufanywa kwa kuzingatia msingi wa maadili na weledi, hali itakayosaidia kumaliza kasoro na changamoto zilizopo hivi sasa katika utoaji wa huduma za afya.

Alisema zipo taarifa za uwepo wa baadhi ya wauguzi wanaofanya kazi bila kuzingatia maadili ya kazi zao, hali inayosababisha wanaohitaji huduma kujikuta katika mazingira ya kupata matatizo zaidi ya yale yaliyowapeleka hospitalini.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, John Matara alisema mbali na mafanikio kiliyoyapata chuo hicho bado kinakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vifaa vya kufundishia pamoja na walimu.

Matara ameomba Serikali na wadau wa sekta ya afya kunusuru hali hiyo kwa kuchangia michango mbalimbali itakayosaidia ujenzi wa majengo ya kisasa yanayoendana na hadhi ya elimu itolewayo katika chuo hicho.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi