loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mollel atoa mil. 9/- Miss Arusha

Mollel atoa mil. 9/- Miss Arusha

Mollel aliwaita wafanyabiashara wenzake sita katika viwanja vya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC), Tawi la Arusha ambako Kampuni ya Monaban imekodishiwa kinu hicho kwa lengo la kuwasaidia warembo hao ikiwa ni njia mojawapo ya kutaka warembo hao kusaidiwa na kujitegemea katika maisha yao ya baadaye.

Mkurugenzi huyo aliagiza viongozi wa warembo hao akiwemo mwakilishi kutoka benki ya CRDB kuhakikisha kila mrembo anafunguliwa akaunti na kuwekewa Sh 600,000 kama kichocheo cha kujituma.

Alisema lengo la kukusanya marafiki zake na kufanya harambee hiyo ni kutaka kila mrembo aliyeshiriki Miss Arusha ajipatie ajira kwa kujiajiri ikiwamo kupewa fedha kidogo kama kianzio cha mtaji.

“Mimi na marafiki zangu tumeamua kufanya harambee hii kwa ajili ya kuwakwamua warembo kiuchumi ili wakimaliza mashindano waweze kujiajiri na waache kuwa tegemezi,” alisema.

Mbali ya hilo, Mkurugenzi wa Monaban aliwataka warembo wa Mkoa wa Arusha kufanya kila linalowezekana kuhakikisha taji ya Miss Tanzania linarejea tena mkoani Arusha kwani warembo wote wana sifa iliyotukuka hivyo wanastahili kuwa Miss Tanzania.

Mollel alisema mara ya mwisho Taji la Miss Tanzania lilichukuliwa na mrembo wa Mkoa wa Arusha, Saida Kessy mwaka 1997, ni muda mwingi umepita hivyo taji hilo linapaswa kurudishwa tena Arusha.

Kwa niaba ya wenzake, Neema Lyimo alimshukuru Mollel na marafiki zake kwa kuwajali na kuwasaidia na kuwataka wafanyabiashara wengine kuiga ili wao walitangaze Jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi