loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Morocco atupiwa virago Oljoro JKT

Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa timu hiyo, Alex Mwamgaya alisema uongozi umechukua hatua hiyo baada ya kuona hali ya mwenendo na uwezo wa kocha huyo kuinusuru timu ishishuke daraja ni mdogo.

Mwamgaya alisema uongozi umeangalia vitu vingi ikiwemo uwezo wake wa ufundishaji na mambo mengine muhimu hivyo umeona kuwa kocha huyo hana jipya na hawezi kuinusuru timu isishuke daraja.

“Tumekuwa tukimfuatilia sana, lakini hali inakuwa mbaya…hivyo tumeona ni bora tusitishe mkataba wake na tutafute kocha mwingine wa kuweza kuinusuru timu iliyokuwa katika nafasi mbaya,” alisema Katibu huyo ambaye timu yao inakamata mkia katika Ligi Kuu.

Hata hivyo, kocha Morocco alipopigiwa simu kuzungumzia hilo, alisema si kweli kuwa ametimuliwa, bali yeye ndiye aliyeamua kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo.

Morocco alisema alifikia uamuzi huo ni baada ya kukosa ushirikiano kutoka viongozi wa juu wa timu hiyo, kitu ambacho ni hatari katika soka na katika hali ilipo timu katika msimamo.

Moroco alisema kabla ya kuingia mkataba wa kuifundisha timu na aliyekuwa Mkuu wa kambi ya JKT Oljoro, Omari Mmari kuna vitu vingi walikubaliana lakini hakuna hata kimoja kilichotekelezwa.

“Mimi ni mtaalamu na mwalimu wa soka na ninajiamini na kamwe sijafukuzwa, ila nimeachia ngazi mwenyewe baada ya kuona hakuna ushirikano katika timu,” alisema kocha huyo wa zamani wa Coastal Union na timu ya Taifa ya Zanzibar.

Alisema mbali ya yeye pia kuna wachezaji wengi wa timu hiyo muda wowote wataikimbia timu hiyo kwa kuona mambo ya uongozi yanakwenda ndivyo sivyo na katika soka hakuna kificho.

Katika hatua nyingine, Ligi Kuu inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Ruvu Shooting Stars dhidi ya ndugu zao wa JKT Ruvu utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi