loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mourinho ataimudu PSG, asema Hazard

Baada ya kuiondoa Galatasaray katika raundi ya mtoano ya timu 16, Blues hao watasafiri kwenda nchini Ufaransa katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo Jumatano ijayo, kabla ya kurudiana Aprili 8 mwaka huu.

Hazard, ambaye amefunga mabao 16 katika michuano yote msimu huu, pia anahisi kwamba PSG wanacheza staili kama ya wapinzani wao wa Ligi Kuu, Arsenal, ambao Jumamosi iliyopita waliwanyuka mabao 6-0.

"Nafikiri kocha ana uwezo mkubwa wa kuweza kuzikabili mechi kama hizi. Tunatakiwa kuwa imara zaidi kwenye safu ya ulinzi," amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubeligiji akiiambia televisheni ya Canal.

"Tunajua kwamba Paris wanapenda kucheza staili kama ya Arsenal: Paris wanacheza soka zuri; Paris wanatawala mchezo. Lakini kama tukicheza kwa kasi tutawashinda tu.”

Aidha alisema si rahisi kumtaja mchezaji bora wa PSG, kwani kikosi hicho kinachonolewa na kocha Laurent Blanc kina wachezaji wengi wa daraja la juu na wenye vipaji vya ukweli.

"Ni kweli kwamba Zlatan Ibrahimovic ni bora zaidi, lakini kikosi chote kina wachezaji wazuri," alisema winga huyo.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi