loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Moyes akataa kutema ubingwa

Moyes ambaye kikosi chake kimebaki katika nafasi ya saba katika msimamo, alisema:

“Ambacho hatutakifanya ni kukubali kusalimu amri kwamba hatuwezi kufika pale. Kazi ni kumaliza wa kwanza na tutajaribu kufanya hivyo.”

Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho alikataa kuiondoa United katika mbio za ubingwa – lakini itahitajika kupoteza mwelekeo kwa moja ya timu zilizo juu yake ili kuipa matumaini ya ubingwa. Alisema:

“Naamini David hatasikitishwa nami kama nitamueleza ukweli. Ni tofauti ya pointi 14 kwa Arsenal, kisha 13 kwa Manchester City na 12 dhidi yetu. “Itahitaji timu tatu kupoteza mwelekeo, kwa hiyo taji litakuwa gumu kwao. Ninachotumaini ni kuwa watazishinda timu nyingine na kumaliza katika nafasi nne za juu.”

United ilianza vyema mechi ya juzi lakini ilifanya makosa katika ulinzi na kumfanya Eto’o kuwa mchezaji wa nne kufunga mabao matatu katika mechi moja katika zama za Ligi Kuu.

Kipigo hicho pia kimemfanya Moyes kuendelea kusubiri ushindi dhidi ya ‘timu nne’ kubwa katika Ligi Kuu.

Katika mechi 48 za ugenini dhidi ya United, Chelsea, Liverpool na Arsenal – ukijumuisha alipokuwa kocha wa Everton na sasa Arsenal – ametoka sare 18 na kupoteza 30. United iko pointi sita kutoka katika nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa zikiwa zimebaki mechi 16. “Huu ni mradi,” aliongeza Moyes.

“Nafahamu nini nitakachofanya na kutakuwa na mabadiliko wakati tunapoendelea na safari. “Ni changamoto kubwa. Nina matumaini tutakuwa katika nafasi nzuri kuliko sasa, lakini hatuko hapo.”

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi