loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mpinzani wa Miyeyusho kuwasili leo

Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa pambano hilo Mussa Kova alisema bondia huyo ataambatana na Kocha wake Amogo Samson, wakitokea nchini kwao kwa ajili ya pambano hilo.

“Pambano limeiva na kesho (leo) tunapata ugeni tayari kwa pambano kali, kila kitu kiko vizuri tunasubiri kuona nani atakuwa bingwa,”alisema. Alitaja viingilio vya pambano hilo kuwa ni Sh10,000 na sh 20,000.

Kova aliongeza kuwa licha kutaja viingilio hivyo maandalizi yanaendelea vizuri kama yalivyopangwa.

Alisema kuwa katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambayo atayatangaza kesho katika mkutano maalumu na vyombo vya habari. Kova alisema pambano hilo litasimamiwa na Chama cha Ngumi za kulipwa Tanzania (PST).

“Mabondia wote wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea Miyeyusho atafanya vizuri na kukabiliana na upinzani wa mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye kiwango cha juu,” alisema Kova.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi