loader
Picha

Mpowora AMCCOS yavuka lengo ukusanyaji wa mazao

Mwenyekiti wa Chama hicho Joseph Kidando alisema wamefanikiwa kukusanya tani 800 kutoka tani 300 zilizokusudiwa kukusanywa kutoka kwa wanachama wake.

Akizungumza na wanachama wa Chama hicho kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Chama uliofanyika kwenye ukumbi wa Mision Ndanda mjini hapa alisema hali hiyo imesaidia kukuza pato la Chama.

Kidando aliongeza kuwa Chama kimeweza kuendesha biashara ya ununuzi wa korosho kwa mtaji wa mkopo kutoka benki ya CRDB na kufanikiwa kurejesha mkopo huo vizuri, aidha Chama kimeweza kuwalipa wakulima wote waliouzia korosho zao ndani ya Chama kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, malipo hayo ni yale ya kwanza, ya pili na malipo ya majaliwa ya Sh 225.

“Mafanikio haya yanajidhihirisha wazi kupitia taarifa tulizoziweka wazi kwenye mbao zetu za matangazo ambazo zinaonesha wazi juu ya uendeshaji wa Chama chetu ambacho kwa sasa tumekuwa Chama cha nne kati ya vyama 34 vilivyopo wilayani Masasi,” alisema Kidando.

Kwa upande wake Ofisa Ushirika Wilaya ya Masasi, Abirahi Mutabazi aliwahimiza watendaji wa chama hicho kuwa na mfumo mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za fedha kwenye vitabu vya fedha.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Hassan Simba, Mtwara

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi