loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msamaha wa kodi kampuni za madini wafutwa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo juzi jioni wakati akisaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya madini ya dhahabu ya Anglogold Ashanti, na Geita Gold Mine, ambazo zitaanza kulipa asilimia nne ya mrahaba.

Alisema kuanzia Januari mwakani kampuni hizo zitatakiwa kulipa kodi kwa kuwa msamaha hautakuwepo na tayari kampuni nyingi zimeanza kulipa kodi ya mapato ya asilimia 30 ya faida, jambo ambalo litaongeza mapato kwa Serikali.

Akizungumzia mkataba huo, alisema kutokana na sheria mpya ya madini ya mwaka 2010 makampuni yote ya madini yanatakiwa kulipa asilimia nne kwa mraba badala ya asilimia tatu iliyokuwa inatolewa hapo awali.

“Serikali ilisaini makubaliano na makampuni ya madini ya mwaka 1999 na kukubaliana kulipa asilimia tatu baada ya kupata faida hivyo kutokana na mabadiliko ya sera ya madini ya mwaka 2009 na sheria ya madini mwaka 2010 watalipa asilimia nne,” alisema.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo migodi yote ya dhahabu inatakiwa kulipa asilimia nne, migodi ya almasi na Tanzanite asilimia tano na kwa sasa wanamalizia majadiliano na mgodi wa Barrick ili wasaini makubaliano hayo ya kulipa asilimia nne kwa mraba.

Profesa Muhongo alisema Halmashauri ya Geita itaanza kunufaika kutokana na kupata dola milioni 1.8 sawa na bilioni tatu kwa mwaka kutoka katika mgodi wa Geita.

Alisema fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa, zisiwe posho za madiwani na halmashauri bali zitumike kuleta maendeleo kwa wananchi.

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi