loader
Picha

MSD waungwe mkono kwa kujenga viwanda vya dawa

Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ukijumuisha magari madogo aina ya LandCruiser 104 na malori 77 aina ya MAN kutoka Ujerumani, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema magari hayo yatasaidia kusambaza dawa hadi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Ilielezwa kuwa, magari hayo yakigawanywa kwa uwiano sawa katika kanda nane za MSD ambazo ni Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tabora, Moshi, Iringa, Dodoma na Mtwara, kila Kanda itapata magari.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Mfuko wa Pamoja (Global Fund) ulitoa msaada wa magari hayo yenye thamani ya Sh bilioni 20.75 ili kusaidia kupunguza changamoto za usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Kutokana na msaada huo, MSD sasa itakuwa na magari 213 kutoka magari 32 iliyokuwa nayo awali.

Kwa mantiki hiyo, tunapenda kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli na wasaidizi wake kwa kuzingatia na kutoa kipaumbele katika huduma za kijamii na hasahasa, huduma za afya na elimu kwa jamii.

Ndiyo maana katika tukio hilo, Rais aliendelea kuwahimiza Watanzania kujenga viwanda vya dawa nchini ili fedha nyingi zinazotolewa kila mwaka kununua dawa na vifaa tiba, zibaki nchini huku pamoja na faida nyingine pia, dawa zipatikane kwa bei nafuu sambamba na upatikanaji ajira kwa watu.

Wakati tukiipongeza Serikali na MSD, tunapenda kuhimiza kuwa, manufaa ya upatikanaji wa magari hayo yanapaswa kuonekana kupitia kupitia upatikanaji wa huduma bora za dawa katika maeneo mbalimbali toka mjini hadi vijijini.

Tunasema kwa upatikanaji wa magari hayo, hatutarajii kuwapo kwa maeneo yatakayokosa dawa eti tu, kwa sababu hakuna usafiri hivyo, ni vema magari hayo kama rasilimali, yawekewe utaratibu mzuri ili yatumike kwa tija, badala ya kuwa nyenzo za usafiri binafsi kwa baadhi ya watu.

Tunasema hivyo tukilenga pia kuwa, MSD sasa ihakikishe inasambaza dawa kadiri ipasavyo kwa kuwa tayari nyenzo za kusafirishia zipo na upatikanaji wa dawa sasa ni wa uhakika.

Ndiyo maana tunasema, tunaipongeza Serikali kupitia MSD na kuwashukuru wadau wote waliowezesha kupatikana kwa magari haya tukisema, yatumike kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuimarisha urafiki baina ya serikali na watu wake.

Tunasema hivyo kwa kuwa tunaamini afya kwa watu ni msingi wa maendeleo katika jamii yoyote kwa kuwa hakuna jamii inayoweza kuendelea, kama afya ya watu wake ina mgogoro.

WATANZANIA juzi walikesha wakishangilia baada ya timu yao ya soka ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi