loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

‘Msidanganyike na wanasiasa waongo’

Makonda alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini hapa, alipokuwa akizungumza na wakazi wa jiji la Mwanza, waliohudhuria kwenye tamasha maalumu la wasanii wa Kanda ya Ziwa.

Alisema baadhi ya wanasiasa, hivi sasa wanatumia katiba kama njia ya kuwarubuni wananchi na kuwasahaulisha kuhoji utekelezaji wa ahadi walizotoa kwenye maeneo yao.

“Nimekaa bungeni siku 67, kazi kubwa tuliyokuwa nayo kwa siku zote hizo ni kutunga kanuni, namna ya kufanya majadiliano na tumejadili Sura ya 1 na 6 ya Rasimu ya Katiba ambazo ndizo zilihitimisha majadiliano yetu katika awamu hii, lakini niwaambieni wakija kwenu wanasiasa kwa mgongo wa Katiba mpya, waulizeni mambo waliyowaahidi ya maendeleo kwenye maeneo yenu,” alisema

Alisema wananchi wakiwahoji wanasiasa wanaojipitisha kwao kwa mgongo wa Katiba, watagundua ni zipi mbivu na mbichi hususani kwa wale walioahidi kutekeleza ahadi zao na hawakufanya hivyo.

Alisema baadhi ya wanasiasa wamejikita katika kudai iandikwe Katiba mpya, tofauti na mataifa makubwa duniani katika nchi za Marekani na India, ambazo zimepata uhuru miaka mingi iliyopita, lakini hazijawahi kuandika upya katiba zao, bali zimekuwa zikifanya marekebisho.

“Katiba ya Marekani ya mwaka 1776 ina kurasa chache na wao hawajawahi kutunga katiba mpya na hata ile ya India, bali wamezifanyia marekebisho machache sana, lakini licha ya sisi kufanya marekebisho katika Katiba yetu yenye ibara 152 imefanyiwa marekebisho mara 18, lakini bado wapo watu wanahitaji katiba mpya na Serikali tatu,” alisema

Alisema binafsi angependa kuona mfumo wa siasa nchini, unajikita katika kujenga uchumi wa nchi, ambao utasaidia pia katika kuinua hali za maisha ya wananchi.

Alisema yangefanyika marekebisho ya mambo ya msingi ya wananchi katika Katiba ya sasa.

Aliwataka wasanii nchini kujitambua kwa kujenga nguvu ya pamoja, waweze kujiinua katika kazi ya sanaa, ambayo alisema inaisaidia Serikali kujitangaza ndani na nje ya nchi.

Katibu wa Chama cha Wasanii wa Filamu mkoa wa Mwanza, Hussein Kim alimuomba Mjumbe huyo wa Bunge Maalumu la Katiba, kuwasilisha kilio chao kwenye mabunge ya Katiba na bajeti ili waweze kutunga Sheria ya hatimiliki ya kulinda mali na kazi za wasanii zisizoshikika .

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi