loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Msijifanye mnajua kufuga samaki'

Ofisa Mtafiti, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi, wizarani hapo, Hakim Matola alisema hayo Dar es salaam na kuongeza kuwa ufugaji samaki hauhitaji gharama kubwa.

Alisema ili kufuga kwa njia iliyo endelevu, ni vyema wananchi wanaotaka kufuga kuhakikisha wanawaona wataalamu wenye ujuzi stahiki kuanzia awamu ya mwanzo.

Alisema katika kuhakikisha ufugaji unaboreka nchini, Wizara inasimamia mradi wa kuzalisha chakula cha samaki wanaofugwa kwa gharama nafuu lengo likiwa ni kuhamasisha wafugaji wa kawaida kufuga kwa manufaa yao wenyewe.

Alisema mradi huo unatekelezwa katika mji wa Songea, Morogoro na Dar es Salaam.

“Chakula hicho kinatengenezwa na bidhaa za kawaida kama pumba, damu ya ng’ombe na hata vidonge vya vitamini ambavyo kwa pamoja mfugaji anapaswa kuelewa namna ya kulisha mifugo hiyo,” alisema Matola.

Alisema mradi huo ambao ni wa miaka miwili unalenga kuhakikisha kila mfugaji anaweza kuvuna samaki mwenye kilo moja katika miezi mitano.

Matola alisema hadi sasa katika eneo la Dar es salaam kuna samaki 200 na wapo wavuvi 10 kutoka kila eneo ambao wamethibitishwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Kuhusu sababu za kuanzisha mradi huo alisema ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wafugaji kutotoa chakula nafuu ambacho wanaweza kuwalisha samaki na kuweza kukua na kuwasaidia kuinua uchumi.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi