loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

‘Msitumiwe na wanaosaka urais’

Mwito huo ulitolewa jana na Shehe Issa Nassoro wakati akitoa hotuba kwenye swala ya Idd el-Fitr iliyofanyika kwenye viwanja vya Ukombozi mjini hapa.

Shehe Issa alisema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa na tabia ya kuwachochea wananchi, hususan vijana, kufanya vurugu na maandamano bila sababu zozote za msingi; ikiwa ni moja ya juhudi zao za kusaka urais na nyadhifa nyingine mbalimbali nchini katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa iwapo wanasiasa wa aina hiyo watapewa nafasi na kutokemewa ipasavyo, wanaweza kusababisha vurugu na kutoweka kwa amani na utulivu uliopo hivi sasa.

Alisema kuwa ni vema wananchi wa kawaida wakaelewa kuwa kama kutatokea vurugu na machafuko yoyote, wao ndio watakaoathirika zaidi kwani wanasiasa watakimbilia nje ya nchi na familia zao.

Kiongozi huyo wa dini ya Kiislamu alisisitiza juu ya umuhimu wa kuheshimiana na kuvumiliana miongoni mwa waumini wa dini zote badala ya kubezana na kukejeliana, hali aliyodai inaweza kuvunja mshikamano.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewashauri watendaji ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi