loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtanzania aingia fainali Madola

Baynit akiwa katika kundi la pili la mchujo, alishika nafasi ya tano, akifuzu kwa fainali kwa kuwa na muda mzuri.

Alitumia dakika 3:40.93. Mwingine aliyefuzu kwa kutumia muda mzuri katika kundi hilo ni Ronald Musagala wa Uganda aliyetumia dakika 3:41.24.

Walifuzu kwa kushika nafasi nne za kwanza katika kundi hilo la A ni Nick Willis (New Zealand) dakika 3:40.76, Jeffrey Riseley (Australia) 3:40.79, James Magut (Kenya) 3:40.79 na Chris O’hare (Scotland) 3:40.80.

Baynit na wenzake hao watano pamoja na washindi wengine sita wa Kundi B walitarajiwa kucheza fainali jana jioni. Katika Kundi B, mwanariadha mwingine wa Tanzania, Dotto Ramadhani Ikangaa alishindwa kufurukuta baada ya kushika nafasi ya 10, hivyo kushindwa kuingia katika fainali.

Ikangaa alitumia dakika 3:46.29, huku aliyeongoza kundi hilo, Mkenya Ronald Kwemoi akitumia dakika 3:39.90. Mkenya huyo alifuatiwa na Charlie Grice (England dakika 3:40.09, Johan Cronje (Afrika Kusini), 3:40.17, Chris Gowell (Wales) 3:40.30 ambao walifuzu kwa kushika nafasi nne za juu, wakati waliofuzu kwa muda mzuri ni Julian Matthews (New Zealand) 3:40.33 na Elijah Manangoi (Kenya) 3:41.63.

Tanzania ambayo haijapata medali hadi sasa, iliendelea kupata matokeo mabaya baada ya wanariadha wake wengine wawili, Fabiano Sulle na Wilbaldo Malley kushindwa katika mbio za mita 10,000.

Sulle alishika nafasi ya 14 katika mbio za mita 5,000 akitumia dakika 13:44.65 ambao ni muda bora kwa mwanariadha huyo, lakini alishindwa kufua dafu katika mbio hizo za juzi za mita 10,000, kwani hakukimbia na haijulikani kwa nini.

Mwenzake, Malley ambaye alikuwa wa 18 katika mbio za mita 5,000, safari hii alikuwa wa 17 akitumia dakika 28:51.94. Katika baiskeli, Thomas Mollel na Richard Laizer watashiriki katika mbio za barabarani za kilometa 170 zitakazofanyika leo.

Mbali na riadha na baiskeli, Tanzania ilipeleka pia timu za mpira wa meza, ndondi, kuogelea, kunyanyua vitu vizito na judo ambazo zimevurunda.

Timu ya Tanzania iliagwa na Rais Jakaya Kikwete na aliwataka kurudi na medali ili kulipa deni wanalodaiwa na Watanzania wenye kiu ya medali baada ya kuzikosa kwa muda mrefu.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi