loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtende Rangers yabugizwa 3-0

Pambano hilo la pekee lililochezwa juzi uwanjani hapo, lilitoa hisia tofauti kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo huku kila mmoja akishindwa kuamini matokeo hayo.

Mtende Rangers ambayo ilikuwa iliongoza ligi hiyo kwa muda kabla ya kuondolewa na Miembeni, ilishuka uwanjani hapo ikiwa na matumaini makubwa ya kushinda ili irudi kileleni, lakini mambo yaliwageukia na kujikuta wakiondoka watupu tofauti na walivyotarajia.

Kwa matokeo hayo, Chuoni imefikisha pointi 23 na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaongozwa na Miembeni yenye pointi 24, huku Mtendea Rangers ikiendelea kushika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi zake 24 ikizidiwa kwa mabao ya kushinda na kufungwa na wanaoongoza ligi hiyo.

Mabao ya washindi hao juzi yaliwekwa kimiani na Bakari Ayoub aliyezifumania nyavu mara mbili katika dakika ya 17 na 54 na Hussein Rashid aliyefunga dakika ya 31.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi