loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtibwa Sugar yaizamisha Ashanti 2-1

Baada ya bao hilo, Mtibwa Sugar walizinduka na kuanza kuliandama lango la Ashanti United na kusawazisha bao hilo lililofungwa na Abdallah Juma dakika ya 38.

Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1 na kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ya wachezaji watano kila moja na kufanya mchezo kuwa wa kushambuliana.

Kila timu ilijitahidi kulinda lango lake huku ikitafuta upenyo wa kushambulia pia na dakika ya 86, Mtibwa Sugar walipata bao la ushindi lililofungwa na Mohamed Mkopi aliyetokea benchi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ashanti United, Abdallah Kibadeni alisema timu yake imefungwa kimchezo na anashukuru amepata mechi zilizompa mwelekeo wa kupata kikosi cha kwanza.

ā€œNashukuru nimeona mwelekeo wa kupata kikosi changu na leo huu ndio mchezo wangu wa mwisho kabla ya kucheza na Yanga Januari 25,ā€ alisema Kibadeni.

Wakati Yanga wakirejea leo kutoka Uturuki walipokuwa wameweka kambi, Ashanti United wao wameweka kambi yao Bamba Beach Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi