loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtoto afa kisimani Dar

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema tukio hilo ni la jana saa 9 alasiri, maeneo ya Keko Magurumbasi Wilaya ya Temeke.

Alisema mtoto huyo alitumbukia wakati alipokuwa akicheza na watoto wenzake maeneo ya nyumbani kwao wakati mama yake akiendelea na shughuli zake.

Alisema kelele za watu waliomwona mtoto huyo ndani ya kisima, zilimshitua mama huyo aliyeungana na majirani lakini jitihada za kuokoa maisha ya mtoto huyo zilishindikana baada ya kufa muda mfupi alipofikishwa katika Hospitali ya Temeke. Maiti amehifadhiwa hospitalini hapo.

Katika tukio jingine, Polisi imewakamata watu 35 wakiwa na bangi kete 17 na pombe haramu ya gongo lita 19.

Kamanda Kiondo alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4:00 asubuhi katika eneo la Keko Machungwa Wilaya ya Temeke wakati Polisi wakifanya msako maeneo hayo.

Aliwataja waliokamatwa katika msako huo kuwa ni James Daniel (37), Alyoce Komba (44), Deborah Jimmy (33) Suma Said (30), Mwajuma Mohammed (39) na wenzao 30.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amemteua Lucas ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi