loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtoto atuhumiwa kumuua mwenzake kwa fimbo

Mtoto huyo (jina tunalihifadhi) anatuhumiwa kumuua mwenzake ambaye naye tunahifadhi jina lake, kwa kumpiga na fimbo kichwani walipokuwa wakichungia ng’ombe hadi kufa baada ya kutokea ugomvi baina yao.

Taarifa kutoka wilayani hapa zinaeleza kuwa mauaji hayo yaliyotokea juzi saa nane mchana kijijini Kabungu wilayani hapa wakati watoto hao wakiwa vibaruani kuchunga ng’ombe, mali ya mfugaji, Ngasa Udodi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alibainisha kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakichunga ng’ombe, lakini ghafla walianza kutupiana maneno makali kwa muda mrefu na kuanza kupigana kwa kutumia fimbo zao za kuchungia ng’ombe.

Kidavashari alieleza mtuhumiwa, mtoto mkubwa alimzidi nguvu mdogo ambapo alimpiga fimbo za mfululizo kichwani na kumsababishia mauti papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda, muda mfupi baadaye wakazi kijijini hapo waliokuwa jirani na eneo hilo walifika kwenye eneo hilo na kumkuta mtoto mdogo tayari akiwa amekufa ndipo walipolitoa taarifa katika kituo cha la Polisi.

Kidavashari alieleza kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya uchunguzi wa awali kukamilika ili sheria kuchukua mkondo wake.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo mengi ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mpanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi