loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtu mrefu zaidi duniani apata `jiko’

Dibo ametokea Hasaka, Syria na anasema; “Nimepata penzi langu la maisha kutoka kwa Kosen”. Ndoa hiyo imefungwa katika mji wao wa Mardin na Kosen, amevaa suti iliyoshonwa kwa kitambaa cha futi 20 ambacho ni zawadi kutoka Wakala wa Anadolu.

Kosen ambaye amezaliwa Desemba 10 mwaka 1982 na ni mkulima wa kabila la Kurdi amekuwa mrefu alivyo sasa kutokana na uvimbe kuathiri tezi ubongo. Kutokana na urefu huo analazimika kutumia magongo kuweza kutembea vizuri.

Kosen hakuwa mrefu sana hadi alipofika miaka 10 ndipo akaanza kurefuka kwa kasi na baadaye akagundulika kuwa na uvimbe kwenye tezi ubongo unaosababisha arefuke kwa kasi, apatwe na maumivu kwenye viungio vya magoti kutokana na kuwa dhaifu.

Kosen anaishi na wazazi wake, kaka zake watatu na dada yake ambao wote wana urefu wa kawaida. Urefu wake umemfanya asiweze kumaliza shule na hivyo kulazimika kufanya kazi kama kibarua mashambani.

Hata hivyo licha ya kuwa mrefu anasema anafurahia maisha yake na anapenda kucheza michezo ya kompyuta na marafiki zake.

Anaelezea faida za kuwa mrefu kuwa ni “ninaweza kuona maeneo ya mbali na kuweza kuisaidia familia yangu katika kazi za nyumbani kama kubadilisha balbu za taa na kubadilisha mapazia bila kupanda kwenye kiti au meza”. Anataja hasara za kuwa mrefu ni pamoja na kukosa nguo, viatu na mashati ya mikono mirefu dukani.

Anavaa viatu saizi 28, mikono mirefu ya mashati inchi 38 na miguu iwe futi 44.4. Kuanzia mwaka 2010, Kosen alipata matibabu ya tezi ubongo katika Chuo cha Afya cha Virginia na baadaye alipewa dawa za kudhibiti kiwango cha homoni za ukuaji ili asiendelee kuwa mrefu.

Matibabu hayo yalitumia miaka miwili na mwaka 2011 kiwango cha homoni zake zilikaa sawa na Machi mwaka 2012 ilibainika kuwa matibabu yake yamefanikiwa. Kosen amenyakua nafasi ya urefu zaidi duniani Agosti 25 mwaka 2009 kutoka kwa Bao Xishun raia wa China, aliyekuwa na urefu wa futi 7 ina inchi 8.9.

Kosen pia anashikilia nafasi ya kwanza ya mtu mwenye mkono mkubwa zaidi duniani ambapo una sentimeta 27.5 na mguu mkubwa zaidi ambapo wa kulia una sentimeta 35.5 na wa kushoto una sentimeta 36.5. Wakati anatangazwa kuvunja rekodi ya Guinness ya kuwa mtu mrefu zaidi duniani, Kosen alisema

“Sikutegemea kama nitaingizwa kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness, nilikuwa naota tu siku zote lakini leo imekuwa kweli”.

Huyo ndio Kosen ambaye kwa miaka 20 rekodi ya Guinness haijawahi kumpima mtu mwenye urefu zaidi yake. Kwa mujibu wa historia ya Guinness watu 10 pekee wamewahi kufikia urefu wa futi nane duniani.

WIZARA ya Viwanda na Biashara imepania ...

foto
Mwandishi: MARDIN, Uturuki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi