loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtuhumiwa wa kesi ya ghorofa Ikulu aonywa

Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo baada ya Wakili wa Utetezi, Henry Massaba kuomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo mpaka tarehe nyingine, kwa kuwa wakili wa mshitakiwa wa pili, Majura Magafu alikuwa Mahakama Kuu akiendelea na kesi nyingine.

Hakimu Fimbo aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 7, mwaka huu, ambapo alimtaka mshitakiwa Richard Maliyaga kuhakikisha katika tarehe hiyo anakuwa na Wakili wake.

"Nilishakwambia kuwa inatakiwa uwasiliane na Wakili wako, si unafika hapa Mahakamani ndiyo unaanza kuwasiliana naye, kesi itakapokuja kutajwa kama hautakuwa na wakili wako, jiandae kujitetea ukiwa mwenyewe," alisema Hakimu Fimbo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake, ambaye ni Maliyaga.

Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 Kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara, karibu na Ikulu, Dar es Salaam.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi