loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtuhumiwa wa milipuko Kilimanjaro Express kukabidhiwa Tanga leo

Milipuko hiyo 475 (baruti) ilikuwa kwenye maboksi matatu makubwa ikisafirishwa kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam ndani ya buti la basi namba T. 491 ARB la Kampuni ya Kilimanjaro Express.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki alisema Januari 11 mwaka huu askari wa doria wa barabara kuu ya Mombo-Segera katika kijiji cha Chekelei cha wilayani Korogwe walikamata mzigo huo.

Aidha alisema kwa kuwa mhusika hakuwepo eneo la tukio ilibidi kutumia mawasiliano ya kiintelijensia kupata taarifa zake ambapo muda mfupi baadae ilibainika kwamba mmiliki wa mzigo huo ni Efatar Mollel anayeishi Kitianjala jijini Arusha.

“Milipuko hii inafanana na ile inayotumika kwenye shughuli za ulipuaji wa miamba na migodi ya madini, lakini tumebaini hii haina chaja (kichocheo) zake za kuwashia ingawa kwa namna ilivyo hapa ikikutana na moto inaweza kulipuka tu kwa urahisi”, alisema.

Alibainisha, “Nasema kwamba milipuko hii imesafirishwa isivyo halali kwa sababu haikuambatana na nyaraka za aina yoyote zinazoweza kuhalalisha mzigo huo… naamini tutakapompata mhusika atatueleza mengi kama anayo leseni pamoja na matumizi hasa ikizingatiwa kwamba Dar hakuna migodi ya uchimbaji madini”, alisema Kamanda Ndaki.

Alisema tayari mtuhumiwa huyo amekamatwa na askari wa mkoani Arusha na sasa taratibu za kumleta Tanga zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Anna Makange, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi