loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Muda wa usajili waongezwa tena

TFF imesema katika taarifa yake jana kwamba kwa mujibu wa CAF, linki hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutoka sasa.

Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili linki hiyo itakapokuwa tayari waingize usajili wao mara moja.

“Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani,” ilisema TFF. “Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (jana Agosti 17, mwaka huu).

Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28, mwaka huu hadi Septemba 3, mwaka huu.

“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili,” ilieleza taarifa ya TFF.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi