loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Muhongo atangaza neema kwa wachimbaji

Pia ametaka uongozi wa kampuni hiyo kushirikiana na vyombo vya habari, kutangaza mazao yanayozalishwa na mgodi huo, kuwezesha kuvutia wakopeshaji na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Aliyasema hayo leo wakati akizindua mkupuo wa kwanza wa uzalishaji wa dhahabu wenye uzito wa kilogramu 25 wenye thamani ya Sh bilioni 1.5.

Dhahabu hiyo ilikuwa kwenye mfumo wa matofali mawili. Uzalishaji chini ya kampuni hiyo, ulianza Julai, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye mgodi huo uliopo katika Kijiji cha Mavota, Kata ya Kaniha, wilayani Biharamulo.

Alisema mgodi huo wa Stamigold utakuwa kielelezo cha historia ya nchi, kwamba Watanzania wamepata elimu bora, utaalamu na wanaweza kuendesha migodi na kuvuna rasilimali zao.

“Mmetufanyia vizuri kwa kutudhihirishia kuwa uamuzi wetu haukuwa wa makosa, maana kuna watu wengi waliutaka mgodi huu na walidiriki kudhihaki kuwa wakipewa Stamico hakutakuwa na tija.

Aliendelea kusema, “Wamezoea kuwa vitu vizuri vinafanywa na wageni au na watu wakutusukuma, nafurahi wote wanaofanya kazi hapa ni Watanzania.”

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico, Dk Alexander Muganda, alisema azma yao kubwa ni kuanzisha miradi ya uchimbaji madini, uchenjuaji na uchongaji ili kupata fedha za kurejesha Hazina na hatimaye mgodi kuweza kujiendesha bila ruzuku ya serikali.

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Stamigold, Denis Sebugwao alisema mgodi huo ulianza uzalishaji wake Julai 15, mwaka huu na hii imedhihirisha kuwa Watanzania wanaweza.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Grace Chilongola, Biharamulo

Post your comments