loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Muswada wa kubana vyombo vya habari waondoshwa

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum ambaye ndiye aliyekuwa mtoa hoja, aliliambia Bunge jana jioni kuwa kuondolewa kwa Muswada huo, kunalenga kwenda kuuboresha kwa kuingiza maoni ya wadau, ambayo hayakuwa yamezingatiwa ipasavyo.

Akitumia Kanuni ya 90 ya Bunge, Waziri huyo alisema serikali itaurejesha Muswada huo baadaye baada ya kuzingatia upungufu uliojitokeza.

Kutokana na kuondolewa kwa Muswada huo, kikao cha Bunge cha jioni jana kiliahirishwa hadi leo asubuhi.

Awali, alisema bungeni kuwa Muswada huo unapendekeza adhabu kwa vyombo vya habari vitakavyochapisha taarifa za kitakwimu za uongo au za upotoshaji.

Kwa mujibu wa Ibara ya 37 (4) ya Sheria hiyo, adhabu itakuwa kifungo cha miezi 12, faini ya Sh milioni 10 au vyote kwa pamoja.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi