loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mv Kigamboni matengenezoni

Aidha huduma za uvushaji watu pamoja na magari zitaendelea kutolewa na vivuko vya Mv Magogoni pamoja na Mv Lami katika kipindi chote cha matengenezo husika.

Ofisa Habari wa Temesa, Theresia Mwami aliliambia gazeti hili jana kuwa wakala huo unaomba radhi kwa usumbufu ambao wananchi wanaotumia vivuko watakaoupata wakati kivuko hicho kitakapokuwa kwenye matengenezo.

Mwami alisema vivuko hivyo havijafanyiwa matengenezo makubwa kwa muda mrefu hivyo kitafanyiwa matengenezo kivuko cha Mv Kigamboni kwanza na baadae Mv Magogoni.

Alisema kivuko cha Mv Lami kina uwezo wa kuchukua abiria 100 na magari madogo 16 wakati kivuko cha Mv Kigamboni kinachukua magari 23 na abiria 800.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi