loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete uungwe mkono

Rais alisema hayo katika taarifa yake, aliyoitoa mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kwanza na wa kihistoria wa viongozi wa Marekani na Afrika, ulioitishwa na Rais Barack Obama wa Marekani.

Mkutano huo ulifanyika kwa siku tatu katika mji wa Washington DC, ambapo pamoja na Tanzania, nchi 47 za Afrika zilialikwa kushiriki. Kupitia mkutano huo, Rais Kikwete alisema Tanzania iko tayari kufanya biashara na nchi hiyo.

Alizitaka kampuni na wafanyabiashara wa Marekani, kuongeza uwekezaji nchini, akisema Tanzania inao uwezo wa kupokea zaidi ya mara 10 uwekezaji wa sasa wa kampuni za Marekani wa dola bilioni 4.5.

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo, kuwa Tanzania inao uwezo mkubwa zaidi wa kufanya biashara kubwa zaidi na Marekani, kuliko biashara ya sasa kati ya nchi hizo mbili zenye thamani ya dola za Marekani milioni 328.8.

Kwetu sisi tunaichukulia fursa hiyo ya kuwepo kwa marais wengi wa Afrika nchini Marekani, kama nafasi muhimu kwetu katika kuutumia mkusanyiko huo, kukaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini.

Hatua ya Rais Kikwete kukaribisha uwekezaji kwenye sekta ya umeme ni hatua muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi nchini, kutokana na ukweli kwamba sekta ya nishati ni injini katika uendeshaji wa viwanda, hivyo iwapo sekta ya ndogo ya umeme itaimarika, uchumi pia utaimarika.

Tunasema hivyo tukiamini kuwa Marekani, kama nchi yenye nguvu kubwa za kiuchumi, inao wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na teknolojia za kisasa, ambao kama wakiamua kuelekeza nguvu zao katika kuboresha sekta ya umeme nchini, bila shaka nchi yetu itapata mafanikio makubwa.

Ni jambo la kufurahisha kwamba Rais Kikwete, anawavutia wawekezaji hao kuja kuwekeza nchini, wakati sekta ya umeme ikiwa katika mapinduzi makubwa ya kutoka utegemezi wa umeme wa maji, kuja katika umeme wa gesi asilia, makaa ya mawe na upepo, hatua ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa na imara.

Mbali ya hilo, Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo, kukaribisha uwekezaji kutoka Marekani wakati ambao Taifa letu kupitia Wizara ya Nishati na Madini, linachukua hatua madhubuti za kuimarisha sekta ya umeme, hatua ambayo imewezesha kuliepusha Taifa kutoka katika kero za mgawo wa umeme, uliokuwa unalikabili kwa kipindi kirefu nyuma.

Ni mategemeo yetu sasa kwamba wafanyabiashara wa Marekani, watautumia mwaliko huo wa Rais Kikwete, kuja nchini na kufanya uwekezaji, hasa kutokana na uwepo wa mazingira mazuri na rahisi ya uwekezaji yanayozidi kuimarishwa na kurahisishwa kila siku na serikali.

Wafanyabiashara wa Marekani hawapaswi kusita hata kidogo, kwani wanayo mifano hai ya namna nchi yetu inavyofanya vizuri katika uendeshaji na usimamizi wa miradi ya kiuchumi, ikiwemo ile ya Malengo ya Milenia (MCC), ambapo Tanzania ni moja ya nchi iliyofanya vizuri katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wake.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi