loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mwanamke Mtanzania 'adaka' Kenya kwa 'unga’

Hayo yamethibitishwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Isebania, Chrispine Kwova. Imeelezwa kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari kanzu wa kituo hicho Alhamisi ya Septemba 4 mwaka huu baada ya kumtilia mashaka alipopekuliwa alikutwa na pakiti zaidi ya kumi za unga unaosadikiwa kuwa wa dawa za kulevya ama kemikali za kutengenezea milipuko.

“Tumetuma sampuli ya unga huo kwa mkemia mkuu jijini Nairobi na mtuhumiwa bado anahojiwa zaidi kuhusu mtandao wake," alisema mtoa taarifa aliyedokeza kuwa, hati ya mwanamke huyo inaonesha amekuwa akifanya safari za mara kwa mara nchi za Ulaya na China, hivyo kumtilia shaka kuwa huenda anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

foto
Mwandishi: Samson Chacha, Tarime

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi