loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwandishi TSN atajwa kuzima uasi

Akitoboa siri hiyo jana katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema kama si vijana hao, huenda mapinduzi yangefanyika na yangefanikiwa, amani ya Tanzania leo isingekuwepo.

Akisimulia ilivyokuwa, Balozi Mahiga ambaye alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa akiwa kijana wa miaka 30, alisema kuna kijana wa miaka 23 aliyekuwa dereva wa teksi (bila kumtaja jina), ambaye alipata taarifa hizo ambazo Serikali haikuwa nazo.

Baada ya kupata taarifa hizo, Balozi Mahiga alisema kijana huyo alimweleza mwandishi wa habari wa Daily News (bila kumtaja jina), ambaye naye alikuwa kijana mdogo wa miaka 27, ambaye alipeleka taarifa hizo kwake.

Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, alipopata taarifa hizo, aliamua kufanya uchunguzi na kubaini kama kweli kulikuwa na mpango wa kutaka kupindua Serikali, ambao waliuzima kwa kukamata washukiwa ambao walipelekwa mahakamani na kufungwa.

Watu hao ambao alisema walisamehewa wakati wa uongozi wa Awamu ya Pili, sasa wapo huru lakini mpango wao kama ungefanikiwa, huenda amani iliyopo sasa isingekuwepo kwa kuwa kuipoteza ni rahisi kuliko kuirejesha.

“Rasilimali kubwa ya amani ni vijana kwa kuwa kama si wale vijana kutoa taarifa, mapinduzi yangetokea na amani iliyopo sasa isingetokea…amani ikipotea ni shida kuirejesha.

“Msiombe kutokee vita…mimi nimeona watu wanaoishi katika vita, hawana hata muda wa kula wala kulala, akifa mmoja mwingine anabeba silaha anaendelea,” alisema Balozi Mahiga.

Alitoa mfano wa taifa la Liberia ambalo ni la kwanza kupata Uhuru katika Bara la Afrika, lakini mwaka 1989 lilipoteza amani kutokana na dhuluma iliyokuwa ikisababishwa na watawala na mpaka leo haijakaa sawa.

Alisema Liberia iliyokuwa ikipokea wakimbizi, ilianza kutoa wakimbizi na sasa inakabiliwa na ugonjwa wa homa kali ya ebola, ambapo Serikali ya nchi hiyo inapata shida kuukabili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kulikosababishwa na kutoweka kwa amani.

Alitoa pia mfano wa Rwanda, ambao baada ya mauaji ya kimbari wakimbizi 200,000 walikimbia nchi yao kuja Tanzania kwa siku moja na baada ya wiki, walifikia wakimbizi milioni moja waliokimbia nchi yao.

Alisema mauaji ya kimbari yalisababishwa na chuki iliyojijenga katika jamii kati ya Wahutu na Watutsi na kuongeza kuwa, namna moja ya kutunza amani, ni kubaini chuki katika jamii na kuziondoa kwa mazungumzo.

Akifafanua kuhusu mwito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kwa Siku ya Amani Duniani, kuwataka walio vitani kuweka silaha chini angalau kwa siku moja ya jana, Balozi Mahiga alisema kama walio katika vita watakubali kuweka silaha chini hata kwa saa moja, kunaweza kutoa fursa ya mazungumzo na kufikia mwafaka.

Siku hiyo ya Amani Duniani mkoani hapa iliadhimishwa kwa mjadala uliokuwa mkali kuhusu amani uliohusisha vijana kutoka shule mbalimbali na katika mashirika mbalimbali nchini.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi