loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mwenyekiti wa CCM Mkoa awapa somo UVCCM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa awapa somo UVCCM

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini Pemba, Abdallah Hamad Mshindo wakati alipozungumza na vijana wanaofanya matembezi ya kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 huko Pemba Chanjanjawiri.

Alisema vijana ndiyo tegemeo la taifa kwa sasa, kwa hivyo wanatakiwa kuijua na kuifahamu historia ya nchi yao ili kuepuka na tabia ya baadhi ya watu kuipotosha kwa maslahi yao.

“Chama cha Mapinduzi kimefurahishwa na matembezi yenu ya kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo sasa uhai wa Umoja wa Vijana umeimarika upya,” alisema.

Akielezea kuhusu Mapinduzi, Mshindo alisema maisha ya wananchi wa kisiwa cha Pemba, sasa yamebadilika sana ambapo karafuu imeleta mabadiliko makubwa ya maendeleo.

Kwa mfano, alisema wananchi wanaoishi vijijini sasa wanafaidika na mavuno ya karafuu, ambapo bei yake imeongezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufikia kilo moja sh 15,000.

“Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yamebadilisha maisha ya wananchi wa Pemba kiuchumi na maendeleo ambapo sasa wakulima wa Karafuu wameneemeka na zao hilo ambalo thamani yake imeongezeka,” alisema.

Aidha alisema Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi ya barabara za vijijini, maji safi na umeme. Alisema miradi hiyo imefungua milango ya uwekezaji Pemba.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi