loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nakumatt kukumbuka shambulizi la Westgate

Mwaka mmoja baada ya shambulio hilo lililotokea katika moja ya maduka ya Nakumatt, menejimenti ya maduka hayo imeamua kufanya sala maalumu katika sehemu zote walipo.

Akizungumzia kumbukumbu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Nakumatt Holdings Atul Shah alisema maduka hayo yote yatachelewa kufunguliwa siku hiyo kwa ajili ya sala maalumu itakayoanza saa tatu asubuhi.

Matawi yote hayo yanatarajia kufunguliwa saa nne asubuhi siku hiyo na baada ya ibada hiyo ya kumbukumbu na itakapofika saa sita mchana itasitisha huduma zake kwa dakika kwa ajili ya kukumbuka waliokufa na kujeruhiwa na shambulio hilo, ambapo katika matawi ya nchini Kenya pia kutapigwa wimbo wa taifa wa nchi hiyo.

Mwaka mmoja uliopita, uongozi wa Nakumatt Holdings ulipoteza wafanyakazi wake watatu katika shambulio hilo ambao ni Veronicah Wairimu, Kennedy Mogaka na John Musango.

Tangu wakati huo, Nakumatt yenye matawi yanayokadiriwa kufikia 50, imeendelea kufungua matawi ya kiwemo yaliyopo mjini Arusha, Moshi na Dar es Salaam, Tanzania.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi