loader
Picha

NBC watangaza faida

Katika ripoti hiyo, mali za jumla ziliongezeka kutoka Sh trilioni 1.6 Machi mwaka huu hadi Sh trilioni 1.7 katika robo ya pili ya kumalizika mwaka huu ambayo ni ongezeko la asilimia tano.

Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo kwa vyombo vya habari, ongezeko hilo linatokana na ukuaji wa amana za wateja wake ulioongezeka kwa asilimia nane kutoka Sh trilioni 1.5 katika nusu ya kwanza ya mwaka jana hadi Sh trilioni 1.7 kwa Juni mwaka huu.

Taarifa hiyo imemkariri Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu, akisema utendaji kazi wenye tija ndani ya miezi mitatu iliyopita, uliwezesha benki kuanzisha bidhaa mpya zenye ubunifu ndani ya soko la kifedha nchini.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mapato yanayotokana na riba yaliongezeka kwa asilimia 15 kutoka Sh milioni 51,524 hadi Sh milioni 55,504 za mwaka huu.

Wakati huo huo benki hiyo imesema imeboresha mtandao wa kibenki unaowezesha wateja kupata akaunti zao na kufanya matumizi ya kifedha popote na wakati wowote.

SERIKALI imezitaka taasisi za kifedha zikiwemo mabenki, kuwekeza katika sekta ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi