loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nchimbi aonya wabunge wenzake

Mjumbe Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ni kiongozi wa kundi la Tanzania Kwanza, alisema msingi wao ni kushiriki katika mchakato huo na kuiacha Tanzania ikiwa moja.

“ Tunataka kushiriki katika kumaliza kazi ya Bunge hili na kuiacha Tanzania ya leo na kesho baada kumaliza ,” alisema Dk Nchimbi.

Aidha, Dk Nchimbi alisema mchakato huo, usiwe sehemu ya kujipatia madaraka, bali iwe ya kuongoza Watanzania katika kuwapatia maendeleo.

Alisema bado watu wana mahitaji makubwa ya huduma za kijamii, kama vile elimu, afya, ufugaji, na miundombinu.

Akifafanua kuhusu suala la kura ya wazi au siri, Dk Nchimbi alisema msimamo wake ni wa kura ya wazi, ambao utajenga mfumo wa maadili ya ukweli na uwazi. Alihoji, “kama wanachangia mjadala kwa wazi, kwa nini kura zisipigwe kwa wazi? Alisema kura ya wazi, itasaidia wananchi kutambua michango yao katika maeneo mbalimbali ilivyowakilishwa.

“Tuko hapa kutunga Katiba ya Watanzania mtu atakumbukwa kwa kile alichokisema,” alisisitiza.

Kwa upande wake, mjumbe, Charles Mwijage alitaka wajumbe wa Bunge hilo kutumia njia ya maridhiano, wanapoona yako mambo wasiyoridhika nayo.

Akizungumzia suala la serikali tatu alisema lina gharama ya uendeshaji, kwani italazimika kuwa na tume nane na kuwa na mabunge matatu yenye viongozi tofauti, ambayo yataongeza gharama.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge hilo, mjumbe kutoka Asasi ya Vijana, Siti Abbas Ali , ambaye pia ni Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), alitaka Watanzania kuondoa hofu juu ya mchakato huo, akisema Katiba hiyo itakuwa ya Watanzania.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi ...

foto
Mwandishi: Magreth Kinabo, Maelezo-Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi