loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Neymar amponza Rais wa Barcelona

“Nimekuwa nikisisitiza mara zote kuwa tulifanya kiusahihi usajili wa Neymar.”

Makamu wa Rais, Josep Maria Bartomeu atachukua madaraka kutoka kwa Rosell, 49. Wiki hii, Jaji wa Mahakama ya Taifa ya Hispania, Pablo Ruz alikubali kesi ya mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases ambaye alidai kuwa kiasi kilicholipwa kilikuwa zaidi ya ada iliyotajwa. Rosell aliongeza:

“Kwa muda sasa, familia yangu na mimi mwenyewe, tumepata vitisho na mashambulio kimyakimya. Vitisho na mashambulio haya vimenifanya nishangae kama kuwa rais kuna maana ya kuhatarisha familia yangu.

“Katika siku za karibuni, tuhuma zisizo na ukweli na haki za matumizi mabaya ya fedha zimeibua kesi dhidi yangu katika mahakama ya Taifa. Tangu mwanzo, nimesema kwamba usajili wa Neymar Junior umefanyika kisahihi na usajili wake umesababisha kinyongo kwa baadhi ya wapinzani wetu.

“Haki ya wanachama kufahamishwa inahitaji kuendana na kulinda klabu na usiri wa baadhi ya mambo na ukweli. Usiri huu ni muhimu katika ulimwengu wa soka kwa sababu vinginevyo klabu itabomolewa.

“Bodi ya Wakurugenzi ni timu. Na timu hii inaongoza mradi ambao umeipatia klabu mafanikio. Sitaki mashambulizi yasiyo ya haki yaathiri menejimenti au taswira ya klabu. Ndio maana nafikiri muda wangu umefika mwisho.

“Sasa, kulingana na Katiba ya Klabu, nimewasilisha kwa Bodi ya Wakurugenzi kujiuzulu kwangu urais wa FC Barcelona ambako hakuwezi kubadilishwa.

“Ilikuwa ni heshima kuwatumikia watu wa Barcelona. Imekuwa heshima kuwa Rais wa FC Barcelona.” Rosell alichaguliwa kuwa Rais wa Barca katika msimu wa 2010 baada ya kupata ushindi wa kishindo kumrithi Joan Laporta, akipata asilimia 62.34 ya kura 57,088 ambayo ni rekodi. Pia aliwahi kuwa Makamu wa Rais chini ya Laporya kabla ya kujiuzulu mwaka 2005.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi