loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NFRA yaongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka

Ofisa Mtendaji Mkuu Charles Walwa alisema leo jijini Dar es Salaam kuwa malengo ya wakala huo ni kuongeza uwezo wa kuhifadhi hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.

Alisema ili kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha, wakala wananunua chakula kutoka kwa wakulima mbalimbali nchini kama vituo vya ununuzi,vikundi vya wakulima, lengo likiwa ni kuhakikisha kunakuwa chakula kinachokidhi mahitaji.

Aliongeza kuwa ili kuchochea uchumi na maendeleo ya Taifa, wakala huo utatoa bei nzuri na ya kuvutia kwa wakulima wanaouza mazao yao kwa wakala.

Alisema kwa sasa wakala umeshalipa Sh bilioni 111.9 kwa wakulima katika mwaka wa fedha 2013/2014.

Walwa alisema Wakala wamekuwa wanatoa ajira za muda mfupi kwa makundi mbalimbali ya jamii, yanayoshiriki katika shughuli mbalimbali za wakala na katika msimu wa wa 2013/2014 wakala umetoa ajira za muda mfupi takribani 3,000.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi