loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ngassa awafunika nyota Afrika

Michuano ya Ligi ya Mabingwa ipo hatua ya nusu fainali sasa ambapo TP Mazembe ya Kongo (DRC) itakutana na ES Setif ya Algeria na AS Vita ya Kongo pia itakutana na CS Sfaxien ya Tunisia.

Yanga ilicheza raundi mbili za awali, dhidi ya Komorozine ya Comoro na dhidi ya Al- Ahly ya Misri. Kwa mujibu wa taarifa ya tathmini iliyotolewa jana kwenye mtandao wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ngassa anaongoza kwa mabao sita.

Katika michuano hiyo, Ngassa alicheza mechi nne za raundi za awali ambapo katika mechi dhidi ya Komorozine alifunga mabao matatu katika kila mechi, nyumbani na ugenini na kufanya idadi ya mabao hayo sita.

Katika mechi ya nyumbani dhidi ya Al- Ahly Yanga ilishinda bao 1-0 lakini ikatolewa kwa mikwaju ya penalti ugenini baada ya Ahly kupata bao moja na kufanya matokeo kuwa sare ya bao 1-1 na hivyo mechi kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Wanaomfuatia Ngassa kwa mabao ni Haithem Jouini (Esperance, Tunisia), Edward Takarinda Sadomba (Al Ahli Benghazi, Libya), Iajour Mouhssine (Raja Club Athletic, Morocco) na Knowledge Musona (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini) wenye mabao matano kila mmoja ambao timu zao pia zimetolewa kwenye michuano hiyo.

Mubele Ndombe wa AS Vita ndiye pekee mwenye mabao matano na timu yake imekwenda nusu fainali.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi