loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ngorongoro waahidi ushindi

Akizungumza jana na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya taifa kwa timu hiyo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Manula ambaye pia anaidakia timu ya Azam alisema lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.

Mechi hiyo ni ya awali kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana wa umri huo.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda akikabidhi bendera hiyo, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano.

Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, hivyo waliopata fursa ya kuwemo Ngorongoro Heroes wakati huu wajue kuwa wamepata bahati, na wanatakiwa kufahamu kuwa wao ni wawakilishi wa Tanzania, na Watanzania wana kiu ya kusikia matokeo ya mechi hiyo.

Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko inaondoka leo saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Shirika la ndege la Kenya ‘Kenya Airways’, na baada ya kuwasili itakwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Garden iliyopo Machakos ambayo ndiyo imepangiwa kufikia na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).

Wachezaji waliopo kwenye msafara huo unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayoub Nyenzi ni Abrahman Mohamed, Aishi Manula, Ally Idd, Ally Mwale, Athanas Mdamu, Ayoub Semtawa, Bryson Raphael na Edward Manyama.

Wengine ni Gadiel Michael, Hamad Juma, Hassan Mbande, Ibrahim Ahmada, Idd Ally, Kelvin Friday, Michael Mpesa, Mohamed Ibrahim, Mudhathir Yahya, Pato Ngonyani, Peter Manyika na Salum Mineli.

Katika hatua nyingine, Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza inaendelea vizuri katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa mitaani yanayoendelea Rio de Janeiro nchini Brazil ambapo katika mchezo wake wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, juzi timu hiyo inayoongozwa na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kutoka Mkoa wa Mwanza, John Kadutu ilicheza mechi mbili ambapo ya kwanza iliifunga Argentina mabao 3-0 na baadaye ikailaza Nicaragua mabao 2-0.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi